Skip to content
البَقَرَة /

Aya 211

2 : 211

Aya 211 of البَقَرَة (2 : 211). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 211

سَلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ كَمۡ ءَاتَيۡنَٰهُم مِّنۡ ءَايَةِۭ بَيِّنَةٖۗ وَمَن يُبَدِّلۡ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Waulize Wana wa Israili: Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi? Na anaye zibadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Explanation & meanings · 1
  1. Waulize Wana wa Israili tumewaletea dalili ngapi za kukata za kuthibitisha ukweli wa Mtume! Na hayo ni neema ya kutaka kuwaongoa wamwendee Mwenyezi Mungu. Lakini wapi! Walizikataa hizo dalili na wakashikilia kuzikanusha hadi ya kuyageuza makusudio yake. Baada ya kuwa hizo dalili ni kwa ajili ya uwongofu zikawa kwa ukafiri wao ni sababu ya kuwazidisha upotovu na kutenda dhambi. Na mwenye kugeuza neema ya Mwenyezi Mungu kwa namna hii basi huyo anastahiki adhabu, na Mwenyezi Mungu hakika ni mkali wa kuadhibu.