Skip to content
البَقَرَة /

Aya 132

2 : 132

Aya 132 of البَقَرَة (2 : 132). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 132

وَوَصَّىٰ بِهَآ إِبۡرَٰهِـۧمُ بَنِيهِ وَيَعۡقُوبُ يَٰبَنِيَّ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰ لَكُمُ ٱلدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسۡلِمُونَ

Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Ibrahim hakutosheka na hayo tu, bali aliwausia wanawe wende mwendo wa uwongofu kama wake. Na mjukuu wake Yaakubu akamuiga, naye akawausia wanawe kadhaalika wafuate mwenendo huo huo. Aliwabainishia wanawe ya kwamba Mwenyezi Mungu amewateulia Dini ya Tawhidi, ya Mungu Mmoja. Na akachukua kwao ahadi kuwa hawatakufa ila nao ni Waislamu, wenye kuthibiti juu ya Dini hii.