19 : 23
فَأَجَآءَهَا ٱلۡمَخَاضُ إِلَىٰ جِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ قَالَتۡ يَٰلَيۡتَنِي مِتُّ قَبۡلَ هَٰذَا وَكُنتُ نَسۡيٗا مَّنسِيّٗا
Kisha uchungu wa kuzaa ukamlazimu kwenda kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliyesahaulika kabisa!