Skip to content
الكَهف /

Aya 78

18 : 78

Aya 78 of الكَهف (18 : 78). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الكَهف Aya 110
Sura · الكَهف
Kiswahili · Barawani
18 : 78

قَالَ هَٰذَا فِرَاقُ بَيۡنِي وَبَيۡنِكَۚ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأۡوِيلِ مَا لَمۡ تَسۡتَطِع عَّلَيۡهِ صَبۡرًا

(Yule mtu) akasema: Huku ndio kufarikiana baina yangu na wewe. Sasa nitakueleza maana ya yale uliyo kuwa huwezi kuyastahamilia.

Explanation & meanings · 1
  1. Mja mwema akasema: Huku kutaaradhi kwako mara kwa mara kwa niyatendayo mimi ndio sababu ya kufarikiana mimi nawe. Sasa basi nitakueleza hikima ya yote haya ambayo wewe huyajui undani wake, wala hukuweza kuyasubiria yaliyo fichikana ukangojea kujua hakika yake na siri yake.