Skip to content
الكَهف /

Aya 48

18 : 48

Aya 48 of الكَهف (18 : 48). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الكَهف Aya 110
Sura · الكَهف
Kiswahili · Barawani
18 : 48

وَعُرِضُواْ عَلَىٰ رَبِّكَ صَفّٗا لَّقَدۡ جِئۡتُمُونَا كَمَا خَلَقۡنَٰكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةِۭۚ بَلۡ زَعَمۡتُمۡ أَلَّن نَّجۡعَلَ لَكُم مَّوۡعِدٗا

Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutakuwekeeni miadi.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Siku hii watu watahudhurishwa kwa makundi wakipangwa kwa masafu kwa ajili ya hisabu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Tumekufufueni kutokana na mauti, kama tulivyo kuumbeni pale mara ya mwanzo. Na mmetujia peke yenu, mmoja, mmoja, bila ya mali, na bila ya wana. Na duniani mlikuwa mkikanusha kufufuliwa na kuhisabiwa.