Skip to content
Al-Kahf /

Aya 14

18 : 14

Aya 14 of Al-Kahf (18 : 14). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Kahf Aya 110
Sura · Al-Kahf
Kiswahili · Barawani
18 : 14

وَرَبَطۡنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ إِذۡ قَامُواْ فَقَالُواْ رَبُّنَا رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَن نَّدۡعُوَاْ مِن دُونِهِۦٓ إِلَٰهٗاۖ لَّقَدۡ قُلۡنَآ إِذٗا شَطَطًا

Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.

Explanation & meanings · 1
  1. Na tulizithibitisha nyoyo zao juu ya Imani na subira ya kuvumilia shida, pale walipo simama mbele ya watu wao wakasema kwa kujifunga kwa ahadi: Ewe Mola wetu Mlezi! Wewe ndiye wa Haki, Mola Mlezi wa mbingu na ardhi! Sisi hatumuabudu mungu mwenginewe. Wala hatutoiwacha itikadi hii. Wallahi! Tukisema jenginelo basi itakuwa tunasema lilio mbali kabisa na kweli!