Skip to content
الإسرَاء /

Aya 93

17 : 93

Aya 93 of الإسرَاء (17 : 93). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 93

أَوۡ يَكُونَ لَكَ بَيۡتٞ مِّن زُخۡرُفٍ أَوۡ تَرۡقَىٰ فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَن نُّؤۡمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيۡنَا كِتَٰبٗا نَّقۡرَؤُهُۥۗ قُلۡ سُبۡحَانَ رَبِّي هَلۡ كُنتُ إِلَّا بَشَرٗا رَّسُولٗا

Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na Mtume?

Explanation & meanings · 1
  1. Au uwe na nyumba iliyo pambwa kwa dhahabu, au upae mbinguni. Na hata hivyo hatukusadiki mpaka ukituletea kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha ukweli wako tukisome! Waambie: Mola wangu Mlezi ametakasika kabisa na kuhukumiwa na yeyote, au yeyote kushirikiana naye katika kudra yake! Mimi si chochote ila ni mwanaadamu kama Mitume wote wengineo. Na wala wao hawakuwaletea watu wao muujiza ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.