17 : 49
وَقَالُوٓاْ أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا وَرُفَٰتًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ خَلۡقٗا جَدِيدٗا
Na walisema: Je! Tutapo kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika, tutafufuliwa kwa umbo jipya?
Explanation & meanings · 1
- Wanao kataa kuwa watafufuliwa wanasema: Hivyo tutafuliwa baada ya kwisha kuwa mafupa yaliyo bunguliwa, na mapande mbali mbali, tukawa hai na umbo jipya? Haya hayaingii akilini.