Skip to content
الإسرَاء /

Aya 25

17 : 25
الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 25

رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمۡۚ إِن تَكُونُواْ صَٰلِحِينَ فَإِنَّهُۥ كَانَ لِلۡأَوَّٰبِينَ غَفُورٗا

Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanao tubia kwake.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi watu! Mola wenu Mlezi anajua kuliko nyinyi yaliyomo katika dhamiri zenu, na atakuhasibuni kwayo kwa thawabu na i'kabu. Na mkiwa mnakusudia wema na mkautenda, tena mkatokea baadhi yenu mkateleza, na kisha mkarejea kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Subhanahu atakusameheni. Kwani Yeye ni Mwenye kusamehe daima kwa wale wanao rejea kwake.