15 : 59
إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
Explanation & meanings · 1
- Wala hakusalimika na huo ukhalifu na adhabu yake ila ahli zake yeye Luut'i. Basi hao Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuwaokoe wote.