15 : 54
قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria?
Explanation & meanings · 1
- Akasema: Vipi mnanibashiria mtoto na hali mimi nimekwisha patikana na udhaifu wa ukongwe. Kwa njia gani, basi, mnanibashiria jambo hili la ajabu?