Skip to content
إبراهِيم /

Aya 7

14 : 7
إبراهِيم Aya 52
Sura · إبراهِيم
Kiswahili · Barawani
14 : 7

وَإِذۡ تَأَذَّنَ رَبُّكُمۡ لَئِن شَكَرۡتُمۡ لَأَزِيدَنَّكُمۡۖ وَلَئِن كَفَرۡتُمۡ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٞ

Na alipo tangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru nitakuzidishieni; na mkikufuru, basi adhabu yangu ni kali.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kumbukeni, enyi Wana wa Israil, pale Mola wenu Mlezi alipo kufunzeni, na akasema: Wallahi! Mkishukuru kwa neema niliyo kupeni ya kukuvueni, na mengineyo, kwa kuthibiti juu ya Imani na ut'iifu, basi hapana shaka nitakuzidishieni neema yangu. Na mkiikanya neema yangu kwa ukafiri na maasi, basi hakika nitakuadhibuni kwa adhabu ya kutia uchungu. Kwani adhabu yangu ni kali kwa wanao kanya.