Skip to content
هُود /

Aya 94

11 : 94

Aya 94 of هُود (11 : 94). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 94

وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا شُعَيۡبٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَأَخَذَتِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ

Na ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Shua'ibu na wale walio amini pamoja naye kwa rehema yetu. Na ukelele uliwanyakua walio dhulumu, na wakapambaukiwa majumbani mwao wamekufa kifudifudi!

Explanation & meanings · 1
  1. Ilipo kuja amri yetu ya kuwaadhibu na kuwaangamiza, tulimwokoa Shua'ibu na walio amini pamoja naye wasipate adhabu na maangamizo. Kuokoka kwao kulikuwa kutokana na rehema iliyo tokana nasi. Ukelele uliwatwaa watu wa Madyana, na tetemeko la kuteketeza, wakapambaukiwa wamekwisha jifia katika majumba yao, wamelala kifudifudi, hawatukusiki hata kidogo!