Skip to content
هُود /

Aya 49

11 : 49

Aya 49 of هُود (11 : 49). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 49

تِلۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهَآ إِلَيۡكَۖ مَا كُنتَ تَعۡلَمُهَآ أَنتَ وَلَا قَوۡمُكَ مِن قَبۡلِ هَٰذَاۖ فَٱصۡبِرۡۖ إِنَّ ٱلۡعَٰقِبَةَ لِلۡمُتَّقِينَ

Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla ya hii. Basi subiri! Hakika Mwisho ni wa wachamngu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hizo ni simulizi tulizo kusimulia wewe, ewe Nabii, juu ya Nuhu na kaumu yake. Hizo ni khabari za ghaibu ambazo hazijui ila Mwenyezi Mungu. Wewe wala watu wako hamkuwa mkizijua kwa namna hii, na kwa tafsili hii, kabla ya wahyi huu. Basi wewe vumilia maudhi ya watu wako, kama walivyo subiri Manabii wa kabla yako. Kwani mwisho wako ni kufuzu kama ulivyo kuwa mwisho wao hao. Na Mwisho mwema daima ni wa wale wanao iogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuamini na kutenda vitendo vyema.