Skip to content
Yunus /

Aya 73

10 : 73

Aya 73 of Yunus (10 : 73). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Yunus Aya 109
Sura · Yunus
Kiswahili · Barawani
10 : 73

فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ خَلَٰٓئِفَ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Wakamkanusha. Basi tukamwokoa, pamoja na walio kuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio walio bakia, na tukawazamisha walio zikanusha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walio onywa.

Explanation & meanings · 1
  1. Na juu ya juhudi hizo, na kukakamia huko aliko kakamia Nuhu kwa ajili ya kutaka kuwaongoa hao watu wake, bado walishikilia kuendelea na kumkanusha na kumfanyia uadui. Basi Mwenyezi Mungu alimwokoa yeye pamoja na wenye kumuamini, wakapanda marikebu. Na akawajaalia hao ndio walio iamirisha nchi baada ya kuteketea makafiri, walio gharikishwa na tofani. Hebu angalia, ewe Muhammad! Vipi walio puuza onyo ulivyo malizikia mwisho wao mbaya.