10 : 53
۞ وَيَسۡتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَۖ قُلۡ إِي وَرَبِّيٓ إِنَّهُۥ لَحَقّٞۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ
Na wanakuuliza: Je! Ni kweli hayo? Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli, na wala nyinyi hamshindi!
Explanation & meanings · 1
- Na makafiri, kwa njia ya kejeli na kukataa, wanakutaka wewe, Mtume, uwaambie hivyo ni kweli hayo uliyo yaleta katika Qur'ani na khabari za kufufuliwa, na adhabu? Waambie: Naam! Kwa haki ya Muumba wangu aliye niumba, hakika hayo yatakuwa bila ya shaka yoyote. Wala nyinyi hamtoshinda wala hamwezi kuzuia adhabu aitakayo Mwenyezi Mungu kukuleteeni.