10 : 50
قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُهُۥ بَيَٰتًا أَوۡ نَهَارٗا مَّاذَا يَسۡتَعۡجِلُ مِنۡهُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Sema: Mwaonaje ikikufikieni hiyo adhabu yake usiku au mchana, sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wakosefu?
Explanation & meanings · 1
- Waambie wanao himiza ifike adhabu: Hebu niambieni, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu usiku au mchana, pana faida gani watayo ipata wakosefu wenye madhambi kutaka ije kwa haraka? Na hali adhabu yote ni mbaya!