10 : 38
أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
Explanation & meanings · 1
- Bali hawa washirikina wanasema: Muhammad kaizua hii Qur'ani mwenyewe! Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa hii Qur'ani ni kazi ya mwanaadamu, basi nyinyi leteni Sura moja tu mfano wake, na muwatake muwatakao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, waje kukusaidieni; ikiwa nyinyi ni wasema kweli katika madai yenu kuwa hii Qur'ani nimeitunga mimi.