Skip to content
يُونس /

Aya 23

10 : 23
يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 23

فَلَمَّآ أَنجَىٰهُمۡ إِذَا هُمۡ يَبۡغُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۗ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَا بَغۡيُكُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۖ مَّتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُكُمۡ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Na akisha waokoa kutokana na khatari ya kuteketea, wanavunja ahadi yao, na mara wanarejea kwenye fisadi walizo kuwa nazo kabla! Enyi watu mvunjao ahadi! Hakika matokeo ya kupindukia mipaka ya starehe na kudhulumu kwenu yatarejea juu yenu peke yenu. Na hakika hizo starehe mnazo zistarehea katika dunia yenu ni starehe za kidunia zenye mwisho. Kisha marejeo yenu ya mwisho ni kwa Mwenyezi Mungu, na Yeye atakulipeni kwa vitendo vyenu mlivyo vitanguliza duniani.