Skip to content
يُونس /

Aya 15

10 : 15

Aya 15 of يُونس (10 : 15). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 15

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَاتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا ٱئۡتِ بِقُرۡءَانٍ غَيۡرِ هَٰذَآ أَوۡ بَدِّلۡهُۚ قُلۡ مَا يَكُونُ لِيٓ أَنۡ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلۡقَآيِٕ نَفۡسِيٓۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۖ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasio taraji kukutana na Sisi husema: Lete Qur'ani isiyo kuwa hii, au ibadilishe. Sema: Hainifalii mimi kuibadilisha kwa nitakavyo nafsi yangu. Mimi sifuati ila ninayo funuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu.

Explanation & meanings · 1
  1. Zilipo dhihiri Aya (Ishara) za Qur'ani kutokana na Mtume wetu Muhammad juu ya washirikina, walisema makafiri wasio ikhofu adhabu ya Mwenyezi Mungu wala hawataraji thawabu zake: Tuletee kitabu kinginecho kisicho kuwa hii Qur'ani. Au badilisha yaliyomo humu, yale yasiyo tupendeza. Waambie ewe Mtume: Hayumkini wala haijuzu mimi kugeuza au kubadilisha kwa nafsi yangu. Mimi si chochote ila ni mwenye kufuata na mwenye kufikisha kile kinacho funuliwa kwangu kutokana na Mola wangu Mlezi. Mimi naogopa, nikienda kinyume na Wahyi, Ufunuo, wa Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku ambayo khatari yake ni kuu, na kitisho chake ni kikubwa!