Skip to content
يُونس /

Aya 101

10 : 101

Aya 101 of يُونس (10 : 101). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 101

قُلِ ٱنظُرُواْ مَاذَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَا تُغۡنِي ٱلۡأٓيَٰتُ وَٱلنُّذُرُ عَن قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ

Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasio amini.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Waambie hawa wenye inda: Tazameni Ishara zilizo wazi zinazo onyesha Ungu na Upweke wa Mwenyezi Mungu zilio enea katika mbingu na ardhi. Lakini Ishara, juu ya wingi wake, na maonyo na yangawa na nguvu, hayawafai kitu watu wanao kataa na wala hawatumii akili zao. Hawa wanao kanya kama hawaamini, basi hawatoangalia. Aya hii na Aya nyingi nyenginezo zinaita watu wajifunze kwa kuangalia na kuzingatia (Observation). Na inaita watu wajifunze ilimu ya ulimwengu na viliomo ndani yake, kwani huo ulimwengu umedhalilishwa kwa ajili ya mwanaadamu. Kisha hizo Aya zinataka watu waingie katika ilimu za kujaribu (Experimental Science). Kwani hiyo ni njia ya kujua kwa kuona vinavyo onekana.