Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 56 kati ya 839

Ondoa vichujio
Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
Upokezi wake ni mzuri رواه ابن ماجه والنسائي في الكبرى وأحمد
Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake asubuhi ya tukio la Akaba huku akiwa juu ya Ngamia wake: "Niokotee kijiwe" Nikamuokotea vijiwe saba, navyo ni vijiwe vya kurusha wakati wa kuwinda, akawa akivipuliza katika kiganja chake huku akisema: "Mfano wa vijiwe hivi basi rusheni" Kisha akasema: "Enyi watu, tahadharini sana na kuchupa mipaka katika dini, kwani kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mpaka katika dini".
Sahihi Imepokelewa na Ibn Majah, Nasai na Ahmad
"Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti".
Sahihi Imepoekelewa na Abu Daud, Nasai na Ibn Majah
"Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake".
Sahihi Imepokelewa na Imamu Ahmad, Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah
"Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka."
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasaai
"Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
"Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ahmad