Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 52 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Birika langu ukubwa wake ni sawa na mwendo wa mwezi mzima, maji yake ni meupe kuliko maziwa, na harufu yake ni nzuri kuliko ya Miski, Vikombe vyake ni kama idadi ya nyota za mbinguni, yeyote atakaye kunywa kwenye birika hilo hatopatwa na kiu milele"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii, kwa utukufu wa yeyote au kwa udhalili wa yeyote, ni utukufu anaoutukuza Mwenyezi Mungu uislamu, na ni udhalili anaoudhalilisha Mwenyezi Mungu ukafiri" na alikuwa Tamimu Dari akisema, nililijua hilo kwa watu wa familia yangu, kwa hakika alipata aliyesilimu miongoni mwao kheri na heshima na utukufu, na aliyekuwa kafiri alipata udhalili na unyonge na ulipaji kodi.
Sahihi Imepokelewa na Ahmad
"Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, na likiwa si la mtu mwema basi husema: Ubaya ulioje, mnalipeleka wapi? Huisikia sauti yake kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angelisikia basi angezimia".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake