Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 4 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Anasimulia yakuwa yeye alikuwa akitoa takbira katika swala zote za faradhi na zinginezo, ndani ya ramadhani na nje ya ramadhani, anatoa takbira anaposimama, kisha anatoa takbira wakati anarukuu, kisha anasema: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema: Rabbanaa walakal hamdu, kabla hajasujudu, kisha anasema: 'Allaahu Akbaru' wakati anapoporomoka kwenda kusujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati anasujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati ananyanyuka kutoka katika kikao kwenda katika rakaa ya pili, na anafanya hivyo katika rakaa zote, mpaka anamaliza swala, kisha anasema anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia msikitini kisha akaingia mtu mmoja, akaswali, kisha akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akajibu salamu, na akasema: "Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali", akarudia kuswali kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja, akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Rudi kaswali kwani wewe hujaswali" (akafanya hivyo) Mara tatu, akasema: "Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivyo, basi naomba nifundishe, akasema: "Utakaposimama katika swala basi toa takbira (sema: Allaahu Akbaru), kisha soma kiasi chepesi ulichonacho katika Qur'ani, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa, na ufanye hivyo katika swala yako yote".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake".
Sahihi Imepokelewa na Ibnu Hiban