Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 110 kati ya 839

Ondoa vichujio

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (48)
"Tambueni kuwa dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyomo, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayompendeza, na msomi, au mwanafunzi".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah
"Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo", Abuu Saidi likamshangaza sana hilo, akasema: Naomba uyarudie tena maneno hayo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akarudia, kisha akasema: "Na la mwisho mja ananyanyuliwa kwalo daraja katika Pepo, umbali ulio kati ya daraja mbili hizo ni kama baina ya mbingu na ardhi", Akasema: Ni lipi hilo ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini, na wala msiwauwe watoto wenu, na wala msilete uzushi mtakouzua kwa mikono yenu na miguu yenu, na wala msiasi katika wema, basi atakayeyatimiza hayo miongoni mwenu basi malipo yake yatakuwa juu ya Mwenyezi Mungu, na atakayetenda lolote katika hayo akaadhibiwa katika dunia basi hiyo ndiyo kafara kwake, na atakayetenda lolote katika hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi hilo litabakia kwa Mwenyezi Mungu akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu" Tukampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, atasema: "Je, mnataka kitu chochote niwazidishie?" Watasema: "Je, hukuziangaza nyuso zetu? Je, hukutuingiza Peponi, na ukatuokoa kutokana na Moto?" Kisha (Mwenyezi Mungu) atainua pazia, basi, hawatapewa kitu chochote kinachopendwa zaidi kwao kuliko kumwangalia Mola wao Mlezi Mwenye Nguvu, Mtukufu."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja, moyo wowote utakaozifyonza basi hutiwa ndani yake doa jeusi, na moyo wowote unaozikataa hutiwa doa jeupe, moyo huo mpaka unakuwa katika (hadhi ya) mioyo miwili, katika weupe mfano wa jiwe jeupe, hivyo hakuna fitina yoyote inayoweza kuudhuru milele kwa muda wote mbingu na ardhi zitakapoendelea kubakia kwake, na moyo mwingine ni mweusi ti! kama chungu kilichofunikwa, haukubali jema, wala haukatai ovu, isipokuwa matamanio ulionyweshwa", Hudhaifa akasema: Na nikamsimulia kuwa hakika kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa, na hivi karibuni utavunjwa, Omari akasema: Hivi utavunjwa? umepata hasara ya kumkosa baba, na lau ungelifunguliwa basi huenda ungelirejeshwa tena, nikasema: Hapana, bali utavunjwa, na nikamsimulia kuwa mlango huo ni mtu atauawa au kufa, na ni mazungumzo ya kweli wala si maneno ya kubumba. Akasema Abuu Khalidi, nikasema kumwambia Saa'di: Ewe Abuu Maaliki nini maana ya nyeusi ti!? Akasema: Ni weupe ung'aao katika weusi, anasema, nikasema: Na nini maana ya chungu kilichofunikwa? Akasema: Kilichogeuzwa juu chini.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika Peponi kuna Soko, watakuwa wakienda hapo kila siku ya Ijumaa, basi utavuma upepo wa kaskazi utawamwagikia katika nyuso zao na nguo zao, na hapo wataongezeka uzuri na urembo, watarudi kwa familia zao wakiwa wameongezeka uzuri na urembo, watasema kuwaambia: Wallahi mmezidi uzuri na urembo baada yetu, watasema: Na nyinyi Wallahi hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".
Sahihi Imepokelewa na Muslim na Ahmad