Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 110 kati ya 839

Ondoa vichujio

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (48)
"Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia".
Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningelifanya kadha basi ingelikuwa kadhaa wa kadhaa, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" hufungua matendo ya shetani".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
“Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu? Akasema: "Usimpe mali yako" Akasema: Wasemaje kama akipigana nami? Akasema: "Pigana naye" Akasema: Wasemaje kama ataniuwa? Akasema: "Basi utakuwa umekufa shahidi". Akasema: Wasemaje kama nitamuuwa? Akasema: "Huyo ataingia Motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?” Akasema: Hapana, isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Hakuna lililotufurahisha zaidi ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Mimi ninampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na ninataraji kuwa pamoja nao kutokana na mapenzi yangu kwao, hata kama nisipofanya sawa na matendo yao.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake