Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 110 kati ya 839

Ondoa vichujio

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (48)
"Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".
Ni nzuri (Hasan) na ni sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa motoni, sijawaona (katika zama zake Mtume), watu walio na mijeledi mithili ya mikia ya Ng'ombe wakiwapiga watu, na wanawake waliovaa na wako uchi, wanenguaji wakatikaji, vichwa vyao ni kama nundu za Ngamia zenye kuyumba (huku na kule), hawa, hawatoingia peponi, na wala hawatoipata harufu yake, na hakika harufu yake hupatikana umbali wa masafa kadhaa wa kadhaa".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah
"Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo".
Amesema Nawawi: Hadithi hii ni sahihi Imepokelewa na katika kitabu cha Al-Hujjah kwa msururu sahihi wa wasimulizi.
"Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (basi malipo yake yatakuwa) ni kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya kuipata dunia, au kwa ajili ya mwanamke atakaemuoa, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kile alichokiendea." Na lafudhi ya Bukhari: ""Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka ,na pambizoni mwa njia kuna kuta mbili, kuta hizo zina milango ilikuwa wazi, na kwenye milango kuna pazia isiyomuonesha mwenyekupita, na mbele ya kila mlango kuna mwenye kuita akisema: Enyi watu, ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na juu ya huyu muitaji kuna muitaji mwingine akiita juu ya njia, na kila mja anapotaka kufungua kidogo milango hiyo anasema: Ole wako wacha usiufungue mlango huo, ikiwa utaufungua tu hutoweza kujizuia, na njia hapa ni Uislamu, na kuta mbili: Ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, na milango iliyofunguliwa: Ni maharamisho ya Mwenyezi Mungu, na huyo muitaji aliyopo mwanzo wa mlango ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muitaji aliyepo juu: Ni Mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu."
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana" Akasema: Haikuwahi kutokea kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, akasema: Wakafunika nyuso zao huku wakitoa sauti za kugugumia (kwa vilio), anasema: Akasimama Omari akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii, anasema: akasimama yule bwana akasema: Ni nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni" [Al-Maaida: 101].
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake