Skip to content

Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii

Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:

"Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii"

«مَنْ لَا يَرْحَمِ النَّاسَ لَا يَرْحَمْهُ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii, huruma ya mja kwa viumbe ni katika sababu kubwa za kupata huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Katika Faida za Hadithi

Huruma inahitajika kwa viumbe wote, lakini wametajwa watu kama sehemu ya kuwapa kipaumbele.

Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa huruma na anawahurumia waja wake wenye huruma, kwani malipo huendana na matendo.

Huruma kwa watu inakusanya kuwafikishia kheri na kuwazuilia shari na kuamiliana nao kwa wema.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (8/ 10) (6013).

Swahiih Muslim (4/ 1809) (2319).

Zaidi (5)

شرح رياض الصالحين.

لابن عثيمين (2/ 553).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (1/ 247).

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (1/ 319).