“Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera
Imesimuliwa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Abi Laila, kuwa, siku moja walikuwa kwa Hudhaifa, akaomba maji, Mmajusi mmoja akampa kitu cha kunywa, alipokiweka kikombe mkononi mwake, akakitupa, na akasema: Kwani si nilishamkataza zaidi ya mara moja au mbili - kana kwamba anasema: Sikufanya hivi kwa matashi yangu - bali nilimsikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake akisema:
“Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera."
«لاَ تَلْبَسُوا الحَرِيرَ وَلاَ الدِّيبَاجَ، وَلاَ تَشْرَبُوا فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ، وَلاَ تَأْكُلُوا فِي صِحَافِهَا، فَإِنَّهَا لَهُمْ فِي الدُّنْيَا وَلَنَا فِي الآخِرَةِ».
Mtume, Rehema na Amani zimshukie, amekataza wanaume kuvaa hariri za kila aina. Aliwakataza wanaume na wanawake kula na kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha. Akasema kuwa ni kwa ajili ya waumini tu Siku ya Kiyama; Kwa sababu waliviepuka katika ulimwengu huu kwa kumtii Mwenyezi Mungu, Ama makafiri wao si vyao huko akhera. Kwa sababu waliharakisha vizuri vyao katika maisha yao ya dunia kwa kuvitumia, na kuasi kwao amri ya Mwenyezi Mungu.
Katazo kwa wanaume la kuvaa hariri na dibaji, na kuwatishia vikali wale wenye kuvaa.
Inafaa kwa wanawake kuvaa hariri na nguo iliyotengenezwa kwa hariri
Uharamu wa kula na kunywa katika sahani za dhahabu na fedha na vyombo vyake, kwa wanaume na wanawake.
Hudhaifa, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alikuwa mkali katika kukemea kwake, na akaeleza hayo kwa kusema kwamba alimkataza zaidi ya mara moja kutumia vyombo vya dhahabu na fedha, lakini hakuacha.
Swahiih Al Bukhaariy (7/ 77) (5426).
Swahiih Muslim (3/ 1638) (2067).
Zaidi (2)
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام.
عبد الله البسام (ص729).
Imenukuliwa katika vitabu
2 VitabuZaidi (2)
- اللآلئ المضيئةعَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى: أَنَّهُمْ كَانُوا عِنْدَ حُذَيْفَةَ، فَاسْتَسْقَى فَسَقَاهُ مَجُوسِيٌّ، فَلَمَّا وَضَعَ القَدَحَ فِي يَدِهِ رَمَاهُ بِهِ، وَقَالَ: لَوْلاَ أَنِّي نَهَيْتُهُ غَيْرَ مَرَّةٍ وَلاَ مَرَّتَيْنِ، كَأَن
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 8«لا تَلْبِسُوا الحَرِيرَ وَلا الدِّيبَاجَ، وَلاَ تَشْرَبُوا في آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ، وَلا تَأْكُلُوا في صِحَافِهَا».