Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, mara kumi (10)
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Ayub -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, mara kumi (10) atakuwa ni kama aliyewaacha huru watu wanne katika wana wa Ismail".
«مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، عَشْرَ مِرَارٍ كَانَ كَمَنْ أَعْتَقَ أَرْبَعَةَ أَنْفُسٍ مِنْ وَلَدِ إِسْمَاعِيلَ».
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir", na maana yake nikuwa: Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu amepwekeka kwa Ufalme uliotimia, na mwenye kustahiki kutajwa na sifa na mapenzi na kutukuzwa pasina mwingine asiyekuwa Yeye, nakuwa Yeye ni muweza hakuna chochote kinachomshinda. Atakayeirejea rejea dhikiri hii tukufu kwa siku mara kumi (10); Basi atakuwa kapata malipo mfano wa malipo ya atakayeondoa utumwa kwa watumwa wanne katika watoto wa Ismail bin Ibrahim -Amani iwe juu yao-, na ametaja kizazi cha Ismail -Amani iwe juu yake-; kwa sababu wao ndio watukufu zaidi kuliko wengine.
Ubora wa dhikiri hii iliyokusanya kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Uungu, na Ufalme, na sifa njema, na uwezo uliotimia.
Thawabu hizi anazipata atakayesema kwa mfululizo au tofauti tofauti.
Swahiih Al Bukhaariy (8/ 86) (6404).
Swahiih Muslim (4/ 2071) (2693).
Zaidi (8)
توضيح الأحكام من بلوغ المرام.
للبسام (7/ 533).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام.
لعبد الله الفوزان (10/ 399).
فتح ذي الجلال والإكرام.
لابن عثيمين (6/ 465).
سبل السلام بشرح بلوغ المرام.
للصنعاني (2/ 703).
Imenukuliwa katika vitabu
4 VitabuZaidi (3)
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"من قال لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك، وله الحمد، وهو على كل شيء قدير عشر مرار. كان كمن أعتق أربعة أنفس من ولد إسماعيل".
- تحفة الأخيار تحفة الأخيار (ببيان جملة نافعة مما ورد في الكتاب والسنة من الأدعية والأذكار)«مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، عَشْرَ مِرَارٍ كَانَ كَمَنْ أَعْتَقَ أَرْبَعَةَ أَنْفُسٍ مِنْ وَلَدِ إِسْمَاعِيلَ» [14]
- شرح الأصول الثلاثة«مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إلَّا اللَّهُ خَالِصًا مِنْ قَلْبِهِ»