Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema:
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakuwa na maneo machafu wala mwenye kuyatafuta, na alikuwa akisema: "Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote".
لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاحِشًا وَلَا مُتَفَحِّشًا، وَكَانَ يَقُولُ: «إِنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أَحْسَنَكُمْ أَخْلَاقًا».
Haikuwa katika tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa na maneno machafu, au vitendo vibaya, na hakuwa anayataka hayo wala kuyatafuta kwa makusudi, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwenye tabia tukufu. Na alikuwa -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Hakika mbora wenu mbele ya Allah ni mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wote, kwa kutenda wema, na kuwa na uso mkunjufu, na kuacha maudhi na kuyavumilia, na kujichanganya pamoja na watu kwa yale mazuri.
...:
Ni lazima kwa muumini ajiweke mbali na maneno machafu na vitendo vibaya.
Ukamilifu wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hayatokei kwake ila matendo mema na maneno mazuri.
Tabia njema ni uwanja wa mashindano, atakayeshinda atakuwa ni muumini bora na mwenye imani iliyokamilika zaidi kuliko wote.
Swahiih Al Bukhaariy (4/ 189) (3559).
Swahiih Muslim (4/ 1810) (2321).
Zaidi (4)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (1/ 672).
تطريز رياض الصالحين.
لفيصل آل مبارك (ص410).
Imenukuliwa katika vitabu
5 VitabuZaidi (5)
- المناهج التعليمية - الصف السادسالمناهج الدراسية - الحديث - الصف السادس - الفصل الأول «لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ ﷺ فَاحِشًا وَلَا مُتَفَحِّشًا، وَكَانَ يَقُولُ: إِنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أَحْسَنَكُمْ أَخْلَاقًا».
- رسالة موجزة عن الإسلام كما جاء في القرآن الكريم والسنة النبوية (مشتملة على الأدلة)رِسَالَةٌُ مُوجَزَةٌُ عَنِ الْإِسْلَامِ كَمَا جَاءَ فِي الْقُرْآنِ الْكَرِيمِ وَالسَّنَةِ النَّبَوِيَّة-مشتملة على الأدلة -للحرمين-«إِنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أَحْسَنَكُمْ أَخْلاَقًا» [45].
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 3«إنَّ مِنْ خِيارِكُم أَحْسَنَكُمْ أَخْلاقاً».
- مشروع المنهج التعليميمادة الحديث مستوى 1لم يَكنِ النبيّ ﷺ فاحِشًا ولا مُتفحّشًا، وكان يقول: «إِنّ من خياركم أحسنَكم أخلاقًا»
- مشروع المنهج التعليميمادة الحديث مستوى 1«إِنّ من خياركم أحسنَكم أخلاقًا».