Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alingia kwangu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikiwa nimeweka pazia lenye picha kwa kusahau, alipoliona akalichana na akaghadhibika mpaka uso wake ukabadilika rangi, na akasema: "Ewe Aisha, Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu" Aisha anasema: "Tukalichana vipande vipande vingine tukavifanya kuwa mto au mito miwili ya kulalia".
دَخَلَ عَلَيَّ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَدْ سَتَرْتُ سَهْوَةً لِي بِقِرَامٍ فِيهِ تَمَاثِيلُ، فَلَمَّا رَآهُ هَتَكَهُ وَتَلَوَّنَ وَجْهُهُ وَقَالَ: «يَا عَائِشَةُ، أَشَدُّ النَّاسِ عَذَابًا عِنْدَ اللهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ الَّذِينَ يُضَاهُونَ بِخَلْقِ اللهِ» قَالَتْ عَائِشَةُ: «فَقَطَعْنَاهُ فَجَعَلْنَا مِنْهُ وِسَادَةً أَوْ وِسَادَتَيْنِ».
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia nyumbani kwake kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake akamkuta akiwa kafunika ghala dogo ambalo huhifadhiwa humo bidhaa kwa kitambaa ambacho kina picha za viumbe hai, ikabadilika rangi ya uso wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa hasira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akalifunua, na akasema: Watu wenye adhabu kali zaidi siku ya Kiyama ni wale wenye kufanya mfano kwa kutengeneza picha za vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu. Aisha akasema: Tukakifanya kitambaa kile kuwa ni mto mmoja au miwili.
...:
Kukemea uovu wakati wa kuuona na kutochelewa katika hilo, madam hakuna madhara makubwa katika hilo.
Adhabu siku ya Kiyama itatofautiana kulingana na ukubwa wa dhambi.
Kupiga picha za viumbe hai ni katika madhambi makubwa.
Miongoni mwa hekima za kuharamishwa kupiga picha za viumbe hai ni kufafanisha vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu, sawa sawa mpigaji awe kakusudia kufananisha au hakukusudia hivyo.
Sheria imetilia umuhimu juu ya kuhifadhi mali kwa kuitumia katika matumizi mengine baada ya kuitoa katika matumizi ya haram.
Katazo la kutengeneza picha za viumbe hai kwa umbile lolote lile litakalokuwa, hata kama litakuwa ni dhalili.
Swahiih Al Bukhaariy (7/ 168) (5954).
Swahiih Muslim (3/ 1668) (2107).
Zaidi (7)
القول المفيد على كتاب التوحيد.
لابن عثيمين (2/ 442).
الملخص في شرح كتاب التوحيد.
لصالح الفوزان (ص399).
الجديد في شرح كتاب التوحيد.
للقرعاوي (ص441).
كتاب التوحيد لمحمد بن عبد الوهاب (ص138).
Imenukuliwa katika vitabu
7 VitabuZaidi (7)
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 3«يَا عَائِشَةُ! أَشَدُّ النَّاسِ عَذَاباً عِنْدَ الله يَوْمَ القِيامَةِ الَّذِينَ يُضَاهُونَ بِخَلْقِ الله».
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 8«يَا عَائِشَةُ، أَشَدُّ النَّاسِ عَذَاباً عِنْدَ الله يَوْمَ الْقِيَامَةِ الَّذِينَ يُضَاهُونَ بِخَلْقِ الله»
- قاموس الكبائر موسوعة الكبائر - المجموعة الأولى«أَشَدُّ النَّاسِ عَذَابًا يَوْمَ القِيَامَةِ الَّذِينَ يُضَاهُونَ بِخَلْقِ اللهِ»[7].
- قاموس الكبائر موسوعة الكبائر - المجموعة الأولى«إِنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَذَابًا عِنْدَ اللَّهِ يَوْمَ القِيَامَةِ المُصَوِّرُونَ» [158].
- قاموس الكبائر«أَشَدُّ النَّاسِ عَذَابًا يَوْمَ القِيَامَةِ الَّذِينَ يُضَاهُونَ بِخَلْقِ اللهِ»[7].
- قاموس الكبائر«إِنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَذَابًا عِنْدَ اللَّهِ يَوْمَ القِيَامَةِ المُصَوِّرُونَ» [158].
- محرمات استهان بها كثير من الناسإن أشد الناس عذابًا عند الله يوم القيامة: المُصوِّرون