Hakika kwako wewe kuna mambo mawili anayapenda sana Mwenyezi Mungu: Upole, na utaratibu
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema:
Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumwambia Ashajji Abdil-Kaisi: "Hakika kwako wewe kuna mambo mawili anayapenda sana Mwenyezi Mungu: Upole, na utaratibu".
قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِلْأَشَجِّ أَشَجِّ عَبْدِ الْقَيْسِ: «إِنَّ فِيكَ خَصْلَتَيْنِ يُحِبُّهُمَا اللهُ: الْحِلْمُ، وَالْأَنَاةُ».
Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumwambia Mundhiri bin Aidhi, Ashajji ni kabila la Abdil-Kaisi na yeye ndiye alikuwa mtemi wao radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Hakika kwako kuna sifa mbili anazipenda mno Mwenyezi Mungu, nazo ni: Akili, kuhakiki mambo, na utulivu, na kutokuwa na pupa.
Himizo la kujipamba na upole utulivu.
Himizo la kuhakiki mambo na kutazama mwisho wake.
Upole na utaratibu ni miongoni mwa sifa nzuri.
Mwenyezi Mungu Mtukufu humsifia mtu kwa sifa alizomuumba nazo miongoni mwa tabia njema.
Ashajju: Ni mtu aliyejeruhiwa usoni, au kichwani, au katika paji la uso.
Swahiih Muslim (1/ 48) (17).
Zaidi (6)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (1/ 681).
تطرز رياض الصالحين.
لفيصل آل مبارك (ص414).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج.
للنووي (1/ 189).