Skip to content

Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto

Kutoka kwa Abuu Absi Abdulrahman bin Jabri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:

"Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto".

«مَا اغْبَرَّتْ قَدَمَا عَبْدٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَتَمَسَّهُ النَّارُ».

Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimbashiria yeyote itakayepatwa na vumbi miguu yake huku akiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa moto hautomgusa.

Katika Faida za Hadithi

Habari njema kwa mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ya kuokoka na moto.

Ametaja miguu miwili pamoja nakuwa vumbi huenea mwili mzima; kwa sababu wapigana ji wengi katika zama hizo walikuwa watembea kwa miguu, na miguu hupata vumbi kwa namna yoyote ile.

Amesema bin Hajari: Ikiwa kitendo cha kuguswa na vumbi pekee kinaharamisha kuguswa na moto; vipi kwa atakayekwenda mbio na akatoa juhudi na akapoteza muda wake.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (4/ 20) (2811).

(2/ 7) (907).

Zaidi (8)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (2/ 424).

التنوير شرح الجامع الصغير.

للصنعاني (7/ 361).

فيض القدير شرح الجامع الصغير.

للمناوي (5/ 437).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (2/ 911).