Skip to content

Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:

"Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia".

«لاَ تَتَّخِذُوا الضَّيْعَةَ فَتَرْغَبُوا فِي الدُّنْيَا».

Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo
Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kujitengenezea makonde na mabustani na mashamba; kwa sababu hilo ni katika sababu za kuipenda sana dunia na kubweteka nayo na kuisahau Akhera.

Katika Faida za Hadithi

Katazo la kukithirisha sana hadhi za kidunia kwa sababu hupelekea kuiacha Akhera.

Katika hadithi hakuna katazo la kutengeneza yale yanayopelekea maisha, bali katazo ni kuzama katika dunia na kuisahau Akhera.

Amesema Sanadi: Na makusudio yake: Nikuwa msizame katika kutengeneza mabustani, mkapumbazika nayo na mkajisahau kumtaja Mwenyezi Mungu.

Rejea

Sunanu Tirmidhiy (4/ 155) (2328).

Musnad wa Ahmad (6/ 54) (3579).

Zaidi (3)

كنوز رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (331/7).

شرح رياض الصالحين لابن عثيمين (375/3).