Skip to content
الأنفَال /

Aya 61

8 : 61

Aya 61 of الأنفَال (8 : 61). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنفَال Aya 75
Sura · الأنفَال
Kiswahili · Barawani
8 : 61

۞ وَإِن جَنَحُواْ لِلسَّلۡمِ فَٱجۡنَحۡ لَهَا وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.

Explanation & meanings · 1
  1. Maadui wakielekea kutaka amani na kuacha uadui wao, basi nawe ewe Mtume, elekea kwenye amani. Kwani vita sio lengo, bali wewe unakusudia kujilinda tu na uadui wao na upinzani wao kupinga wito wako. Basi kubali amani, na umtegemee Mwenyezi Mungu, wala usikhofu vitimbi vyao na njama zao! Yeye Subhanahu ni Mwenye kuzisikia njama zao, ni Mwenye kuijua mipango yao. Hapana kinacho fichikana kwake. Huu ni msingi mkuu katika misingi ya Uislamu, Dini ya Salama. Na leo tunasikia kila dola duniani ina nadi Usalama, na kwa hivyo ukaundwa Umoja wa Mataifa.