Skip to content
المُجَادلة /

Aya 4

58 : 4

Aya 4 of المُجَادلة (58 : 4). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المُجَادلة Aya 22
Sura · المُجَادلة
Kiswahili · Barawani
58 : 4

فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ مِن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۖ فَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ فَإِطۡعَامُ سِتِّينَ مِسۡكِينٗاۚ ذَٰلِكَ لِتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Na asiye pata mtumwa kumkomboa, basi na afunge miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiye weza hayo basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na kwa makafiri iko adhabu chungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na asiye pata mtumwa wa kumkomboa, basi yampasa afunge miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiye weza kufunga hivyo basi itampasa awalishe masikini sitini. Tumeyalazimisha hayo ili mpate kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mtende kwa mujibu wa Imani hiyo. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikiuke. Na makafiri watapata adhabu yenye machungu makali.