Skip to content
الزُّخرُف /

Aya 85

43 : 85

Aya 85 of الزُّخرُف (43 : 85). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الزُّخرُف Aya 89
Sura · الزُّخرُف
Kiswahili · Barawani
43 : 85

وَتَبَارَكَ ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ametukuka na ametaadhamu Yeye ambaye, peke yake, Mwenye ukamilifu wa kutekeleza katika mbingu na ardhi na baina yao katika viumbe vya angani vinavyo onekana na vyenginevyo, na mipango yote iko kwake, na Yeye tu ndiye Mwenye kujua wakati wa Kiyama, na kwake Yeye peke yake, mtarejeshwa mwishoe kwa ajili ya hisabu.