Skip to content
النور /

Aya 64

24 : 64

Aya 64 of النور (24 : 64). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النور Aya 64
Sura · النور
Kiswahili · Barawani
24 : 64

أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قَدۡ يَعۡلَمُ مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ وَيَوۡمَ يُرۡجَعُونَ إِلَيۡهِ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُواْۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ

Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakika Yeye anajua mlio nayo. Na siku mtapo rudishwa kwake atawaeleza waliyo yafanya. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Zindukaneni enyi watu! Mjue kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kumiliki mbingu na ardhi, na viliomo ndani yao. Anayajua mlio nayo, ukafiri wenu na Uislamu wenu, na uasi wenu, na ut'iifu wenu. Basi msiende kinyume na amri yake. Na Yeye atawapa khabari watu, watapo rejea kwake Siku ya Kiyama, kwa yote waliyo yatenda duniani, na atawalipa kwayo. Kwani Yeye amekizunguka kila kitu kwa ujuzi wake.