Skip to content
البَقَرَة /

Aya 181

2 : 181

Aya 181 of البَقَرَة (2 : 181). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 181

فَمَنۢ بَدَّلَهُۥ بَعۡدَ مَا سَمِعَهُۥ فَإِنَّمَآ إِثۡمُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na atakaye ubadilisha wasia baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakao ubadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

Explanation & meanings · 1
  1. Ukitoka wasiya basi huo ni haki iliyo waajibu, haijuzu kuugeuza na kuubadilisha ila ikiwa wasiya huo umeacha uadilifu. Mwenye kubadilisha haki akageuza wasiya muadilifu ulio sawa baada ya kujua hukumu hii basi huyo amepanda madhambi yatakayo mletea adhabu. Mwenye kuusia hana kosa kwa yatakayo tokea baada yake, wala hakudhani kuwa atakuwapo atakaye fanya hayo, wala yeye hapatilizwi kwa hayo. Mwenyezi Mungu, hakika, ni Mwenye kusikia na kujua, wala hapana linalo fichikana kwake.