Skip to content
الإسرَاء /

Aya 69

17 : 69

Aya 69 of الإسرَاء (17 : 69). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 69

أَمۡ أَمِنتُمۡ أَن يُعِيدَكُمۡ فِيهِ تَارَةً أُخۡرَىٰ فَيُرۡسِلَ عَلَيۡكُمۡ قَاصِفٗا مِّنَ ٱلرِّيحِ فَيُغۡرِقَكُم بِمَا كَفَرۡتُمۡ ثُمَّ لَا تَجِدُواْ لَكُمۡ عَلَيۡنَا بِهِۦ تَبِيعٗا

Au mmeaminisha ya kuwa hatakurudisheni humo mara nyengine na kukupelekeeni kimbunga cha upepo akakuzamisheni kwa mlivyo kufuru, na kisha msipate wa kukunusuruni nasi.

Explanation & meanings · 1
  1. Au nyinyi mmeaminisha kuwa Mola wenu Mlezi hatakurejesheni tena baharini, na akuleteeni tufani la upepo livunjilie mbali hicho chombo chenu? Akakuzamisheni kwa sababu ya kuto thamini neema yake pale alipo kuokoeni mara ya kwanza? Tena hapo hamtapata wa kukuteteeni kwetu kwa tuliyo kufanyieni ili mpate kusalimika.