Skip to content
هُود /

Aya 109

11 : 109

Aya 109 of هُود (11 : 109). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 109

فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّمَّا يَعۡبُدُ هَٰٓؤُلَآءِۚ مَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبۡلُۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمۡ نَصِيبَهُمۡ غَيۡرَ مَنقُوصٖ

Basi usiwe na shaka juu ya wanayo yaabudu hao. Hawaabudu ila kama walivyo abudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Ilivyo kuwa hali ya watu washirikina walio dhulumu katika dunia na akhera ni hiyo tuliyo kusimulia, ewe Nabii, basi usiwe na shaka yoyote juu ya mwisho wa hao katika kaumu yako wanao abudu masanamu pindi wakiendelea katika upotovu wao. Kwani hali yao ni hali ya baba zao walio watangulia, ambao khabari zao tumekusimulia. Wote hao ni washirikina. Na Sisi tutawatimizia kwa ukafiri wao adhabu kaamili kwa kadiri ya makosa yao. Hawatapunguziwa hata chembe.