Skip to content
يُونس /

Aya 83

10 : 83

Aya 83 of يُونس (10 : 83). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 83

فَمَآ ءَامَنَ لِمُوسَىٰٓ إِلَّا ذُرِّيَّةٞ مِّن قَوۡمِهِۦ عَلَىٰ خَوۡفٖ مِّن فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِمۡ أَن يَفۡتِنَهُمۡۚ وَإِنَّ فِرۡعَوۡنَ لَعَالٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ

Basi hawakumuamini Musa isipo kuwa baadhi ya vijana vya kaumu yake, kwa kumwogopa Firauni na wakuu wao wasiwatese. Kwani hakika Firauni alikuwa jeuri katika nchi. Na kwa yakini alikuwa miongoni mwa walio pita kiasi.

Explanation & meanings · 1
  1. Na juu ya kudhihiri Ishara zote za kusadikisha Ujumbe, wale walio muamini Musa hawakuwa ila ni kikundi cha watu wachache tu katika kaumu ya Firauni. Waliamini juu ya kuwa wakiogopa asije Firauni na walio pamoja naye wakawaachisha waliyo yaamini. Jeuri za Firauni zilikuwa kubwa mno katika Misri! Hakika yeye ni katika walio pita upeo katika kutakabari na kujivuna.