Skip to content
يُونس /

Aya 11

10 : 11

Aya 11 of يُونس (10 : 11). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 11

۞ وَلَوۡ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسۡتِعۡجَالَهُم بِٱلۡخَيۡرِ لَقُضِيَ إِلَيۡهِمۡ أَجَلُهُمۡۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Na lau kama Mwenyezi Mungu angeli wafanyia watu haraka kuwaletea shari kama wanavyo jihimizia kuletewa kheri, bila ya shaka wangelisha timiziwa ajali yao. Lakini tunawaacha wale wasio tumainia kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao.

Explanation & meanings · 1
  1. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli waitikia watu wanapo jiapizia shari kama vile wanavyo jihimizia kuitaka kheri, angeli waangamiza akawateketeza wote. Lakini Yeye anawachukulia kwa upole basi anaakhirisha kuwateketeza, ili kungojea wadhihirishe walio nayo kwa mujibu wa anavyo wajuulia, upate kuonekana wazi uadilifu wake kwa atavyo walipa. Wanaachwa na ushahidi wa kutosha umesimama dhidi yao, nao makusudi wanakengeuka na kuelekea njia ya upotovu na udhalimu.