Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 130 kati ya 839

Ondoa vichujio

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (58)
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapoondoka katika swala yake anaomba msamaha mara tatu, na anasema: "Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam", Anasema Walid: Nikasema kumwambia Auzaiy: Ni vipi unaomba msamaha: Akasema: Unasema: Astagh-firullaah, Astagh-firullaah.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيأذكار الصلاةموضوعات الحديثالذِّكْر، سنن الصلاة، صفة الصلاة
Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi.
Sahihi Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
التصنيف الشرعيكيف تدخل في الإسلام، موجبات الغسلموضوعات الحديثأحكام الغسلمحاور التعريف بالإسلامما بعد الدخول في الإسلام
"Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
التصنيف الشرعيآداب الأكل والشرب، الاستنجاء وقضاء الحاجةموضوعات الحديثآداب الأكل والشرب، آداب قضاء الحاجة، أحكام الاستنجاء والاستجمار
"Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
التصنيف الشرعيالمجتمع المسلم، فضائل الأعمال الصالحة، الأخلاق الحميدةموضوعات الحديثموالاة المؤمنين
"Hakitosimama Kiyama mpaka apite mtu juu ya kaburi la mtu aseme: Natamani ningekua nafasi yake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
التصنيف الشرعيأحوال الصالحين، تزكية النفوس، أشراط الساعةموضوعات الحديثأشراط الساعة
Mtu mmoja alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini maana ya wawili wenye kustahiki? Akasema: "Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيفضائل التوحيد، توحيد الألوهية، الشركموضوعات الحديثأهمية التوحيد، الشرك بالله وأقسامهمحاور التعريف بالإسلاموجوب إفراد الله بالعبادة، بطلان الشرك وصوره
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
التصنيف الشرعيآداب العطاس والتثاؤب، الهدي النبويموضوعات الحديثالآداب
"Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa".
Sahihi Imepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa
التصنيف الشرعيفضائل السور والآيات، أذكار الصلاةموضوعات الحديثفضائل السور والآيات، سنن الصلاة