Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 10 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji fulani vinavyotengenezwa huko, akasema: Ni vipi hivyo?, akasema: "Ni Bit'u na Mizru" akaulizwa Abuu Buraida: Bit'u ni nini? Akasema: Ni mvinyo wa Asali, na Mizru: Ni mvinyo wa ngano, akasema: "Kila kilevi ni haramu" Ameitoa Bukhari.
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
التصنيف الشرعيالأشربة المحرمة، الأربعون النووية
"Mambo manne yatakayekuwa kwake basi atakuwa mnafiki, ana akiwa na jambo moja miongoni mwa hayo basi atakuwa na tabia ya unafiki mpaka aiache: Yule anayesimulia akasema uongo, na akiahidi hatimizi, na akigombana hupita mipaka, na akiingia makubaliano hufanya hiyana".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
التصنيف الشرعيالأربعون النووية، ذم المعاصي، النفاق
"Yeyote atakayezua (kitu) katika jambo letu hili (dini) ambalo si miongoni mwake, basi hilo litakataliwa."
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
التصنيف الشرعيالبدعة، الأربعون النووية
"kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"
Sahihi Imepokelewa na Muslim, vile vile Bukhari ikiwa na ibara ya mwisho ndani ya kitabu chake
التصنيف الشرعيالأشربة المحرمة، التوبةموضوعات الحديثشرب الخمر
"Kila wema ni sadaka"
Sahihi Imepokelewa na Bukhari kutokana na hadithi ya Jaabir, na amepokea Muslim kutokana na hadithi ya Hudhaifa
التصنيف الشرعيفضائل الأعمال الصالحة، صدقة التطوعموضوعات الحديثحسن الخلق، الإحسان إلى الخلق، صدقة التطوعمحاور التعريف بالإسلاممحاسن الأخلاق
"Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilolinuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi (malipo yake yatakuwa) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya dunia ataipata, au kwa ajili ya mwanamke ili amuoe, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa lile alilolihamia".
Sahihi Imepokelewa na Maimamu wawili wa wanachuoni wa Hadithi, Abu Abdillah Muhammad bin Ismail bin Ibrahim bin al-Mughirah bin Bardizbah al-Bukhari na Abu al-Husayn Muslim bin al-Hajjaj bin Muslim al-Qushayri an-Naysaburi katika Sahih zao mbili, ambavyo ndivyo vitabu sahihi zaidi vilivyotungwa.
التصنيف الشرعيالأربعون النووية، أعمال القلوب
"Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
التصنيف الشرعيالأربعون النووية، وجوب الصلاة وفضلها وحكم تاركها، وجوب الزكاة وحكم تاركها، وجوب الصيام وحكم تاركه، وجوب الحج والعمرة وحكم تاركهما، الإيمان بالله عز وجل، النبوة والرسالة، الإسلام
"Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
التصنيف الشرعيالأربعون النووية، الأنبياء والرسل السابقين عليهم السلام