Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 27 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Alisema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi sisi tutaadhibiwa kwa tuliyoyafanya katika zama za ujinga kabla yakuwa waislamu?Akasema "Yeyote atakayefanya wema katika Uislamu basi hatoadhibiwa kwa yale aliyoyatenda katika zama za ujinga, na yeyote atakaye tenda maovu akiwa katika Uislamu ataadhibiwa kwa makosa yake ya mwanzo na ya mwisho".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
"Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Ya kwamba yeye alisema kumuuliza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Unaonaje ikiwa nitakutana na mtu miongoni mwa makafiri, tukapigana, akapiga moja ya mikono yangu kwa upanga akaukata, kisha akajificha katika mti, akasema: Nimejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, je nimuue ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu baada ya kuwa amelisema neno hilo? Akasema: "Usimuue" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kakata moja ya mikono yangu, Kisha akasema hivyo baada ya kuwa kaukata?! Akasema: "Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bin Jud'aan kabla ya uislamu alikuwa akiunga udugu, na akilisha masikini, je hilo litamfaa?Akasema: "Halitamnufaisha, na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Mtu yeyote atakayesema kumwambia ndugu yake: Ewe kafiri, basi utampata mmoja katika ya hao wawili, ikiwa atakuwa kama alivyosema (litathibiti hilo), na kama si hivyo utarejea kwake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake