Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 10 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kukihifadhi, Makuraishi wakanikataza, na wakasema: Hivi unaandika kila kitu unachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu huzungumza wakati wa hasira na furaha? Nikaacha kuandika, nikamueleza hilo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaashiria kwa kidole chake katika kinywa chake, akasema: "Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapowaamrisha anawaamrisha katika matendo yale wanayoyaweza, wakasema: Sisi hatuna nafasi kama yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, basi anachukia mpaka anaonekana usoni kuwa amechukia, kisha anasema: "Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Nilisafiri katika msafara wa Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
"Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini, akakaa Makkah miaka kumi na tatu, kisha akaamrishwa kuhama, hivyo akahama kwenda Madina, akakaa Madina miaka kumi, kisha akafariki Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu. Nimenusuriwa na hofu kwa umbali wa safari ya mwezi mmoja. Na nimefanyiwa ardhi kuwa mahali pa kuswalia na ni twahara (safi). Hivyo, yeyote katika umma wangu atakapokutwa na swala, basi na aswali (popote). Na nimehalalishiwa ngawira. Na kila Nabii alikuwa akitumwa kwa umma wake tu, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote. Na nimepewa uombezi (Siku ya Kiyama)”.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake