Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 14 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwa sababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi hakika nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja wangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko kile nilichomfaradhishia, na hatoacha mja wangu kuendelea kujiweka karibu yangu kwa mambo ya sunna mpaka nitampenda, nikishampenda nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analoonea, na mkono wake anaokamatia, na mguu wake anaotembelea, na akiniomba hakika nitampa, na akinitaka ulinzi hakika nitamlinda".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake