Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 22 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Tulikuwa tumekaa pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja nasi Abubakari na Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao katika kundi, akasimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake mbele yetu, akaondoka na akachelewa, tukahofia asije kudhuriwa mbele yetu, tukapatwa na hofu tukasimama, mimi nilikuwa wa kwanza kufadhaika, nikatoka nikimtafuta Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake mpaka nikafika katika ukuta wa Answari (watu wa Madina) katika ukoo wa bani Najjar, nikauzunguka ili nipate mahala mlango ulipo, sikuupata! Ghafla nikaona kimviringo kidogo kinachoingia ndani ya ukuta kutokea nje kilipo kisima, nikakifukua, nikaingia kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Akasema kwa mshangao "Nani we, Abuu Huraira?!" Nikasema: Ndiyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Nini kimekuleta?" Nikasema: Ulikuwa umekaa pamoja nasi ukasimama ukaondoka na ukachelewa kurudi, tukahofia usije kudhurika mbele yetu, tukapatwa na mfadhaiko, mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kufadhaika, nikaja katika ukuta huu, nikafukua kama anavyofukua Mbweha, na hawa watu wako nyuma yangu. Akasema: "Ewe Abuu Huraira" Na akanipa viatu vyake, Akasema: "Nenda na viatu vyangu hivi viwili, yeyote utakayekutana naye mbele ya ukuta huu na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi mpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi", akawa mtu wa kwanza kukutana naye ni Omari. Akasema: "Ni vya nini viatu hivi viwili ewe Abuu Huraira?" Nikasema viatu hivi ni vya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, kaniagiza navyo kuwa yeyote nitakayekutana naye na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi nimpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi, Omari akanipiga kibao kwa mkono wake kifuani kwangu kati ya maziwa mawili nikaangukia kisogo changu, akasema: Rudi ewe Abuu Huraira!, nikarudi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikataka kuangua kilio, akanifuatilia Omari naye akiwa nyuma yangu, nilipofika, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake "Umekuwaje ewe Abuu Huraira?" Nikasema: Nimekutana na Omari nikamueleza ulichoniagiza, akanipiga kibao kifuani kati ya maziwa yangu mawili, nikaangukia kisogo, akasema: "Rudi!" Basi akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Omari, ni nini kimekupelekea kufanya ulichokifanya?" Omari akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nakuthamini na niko radhi fidia yako kumtoa baba yangu na mama yangu, hivi ni kweli umemtuma Abuu Huraira akiwa na viatu vyako, kuwa atakayekutana naye hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi ampe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi? Akasema: "Ndiyo nimemtuma", Omari akasema: Ni bora usifanye hivyo, hakika mimi nahofia watu watabweteka na hilo, acha watende, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Basi Abuu Huraira waache".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, anasema: Akatuma mjumbe Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na watu wakiwa mahali pao pa kulala: "Kusibaki katika shingo la mnyama bangili za shaba au kengele isipokuwa (ahakikishe) zimekatwa".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakwamba Mama Salama alimsimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kisa cha kanisa aliloliona katika ardhi ya Ethiopia, likiitwa kanisa la Mtakatifu Maria, akasimulia aliyoyaona ndani yake miongoni mwa picha, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia, na wanachora ndani yake picha hizo, hao ndio viumbe waovu zaidi mbele ya Allah
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini". Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: "Ni neno jema".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu", akasema Omari: Wallahi sikuwahi kuapa tena kwa kiapo hicho tangu nilipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alipokataza hivyo, kwa kutamka mwenyewe wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake